// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GAMBO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA ARUSHA KATIKA ENEOLA HEKARI 15 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GAMBO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA ARUSHA KATIKA ENEOLA HEKARI 15 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, February 02, 2019

    GAMBO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA ARUSHA KATIKA ENEOLA HEKARI 15

    Na Mwandishi Wetu, ARUSHA
    MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kwamba wana mpango wa kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo katika eneo la ukubwa wa hekari 15.
    Gambo ameyasema hayo leo asubuhi wakati akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC) mjini Arusha.
    “Serikali ya Mkoa wa Arusha tumetenga hekari 15 kwa ajili ya kujenga uwanja wa kisasa wa michezo na TFF ndiyo watakaousimamia bila kupata usumbufu,”alisema Gambo.
    Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema watajenga Uwanja wa kisasa katika eneo la ukubwa wa hekari 15

    Akifungua mkutano huo, Gambo aliwataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kuheshimu mamlaka akisema kuwa hata kama kuna mtu haridhiki na utawala wa sasa wa TFF, hana budi kuiheshimu kwani mamlaka hiyo imewekwa kihalali na inatambuliwa na Serikali.
    “Uchaguzi mlishafanya na tunajua safu ya uongozi ilishakamilika lakini bado kuna watu wanataka kuirudisha TFF ilikotoka. Ombi langu kwenu ni msikubali”, alisema Gambo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GAMBO AAHIDI KUJENGA UWANJA WA KISASA ARUSHA KATIKA ENEOLA HEKARI 15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top