SIMBA SC YAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA SPORTPESA, KUMENYANA NA BANDARI
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM SIMBA SC imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Ushindi huo unakuja siku nne baada ya Simba SC kufungwa 5-0 na wenyeji wao, AS Vita mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji Patrick Aussems, itakutana na Bandari ya Mombasa nchini Kenya pia katika Nusu Fainali, wakati FC iliyowatoa mabingwa watetezi, Gor Mahia watamenyana na Kariobangi Sharks iliyowatoa Yanga SC. Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya 13 kwa shuti akimalizia krosi ya beki kutoka Brukina Faso, Zana Coulibally.
Wachezaji wa Simba SC wakishangilia bao lao la kwanza leo Uwanja wa Taifa
Mfungaji wa bao la pili la Simba SC, Clatous Chama akimtoka mchezaji wa AFC Leopards
Emmanuel Okwi akimtoka mchezaji wa AFC Leopards ya Kenya
Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akimtoka mchezaji wa AFC Leopards
Mashabiki wa Simba SC wakifurahi leo Uwanja wa Taifa siku chache baada ya kufungwa 5-0 na AS Vita mjini Kinshasa
Okwi akamsetia kiungo Mzambia, Clatous Chama kuifungia Simba SC bao la pili dakika ya 48 kabla ya Vincent Oburu kuidungia AFC Leopards, zamani Abaluhya bao la kufutia machozi dakika ya 61. Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Aishi Manula, Rashid Juma, Zana Coulibally, Lamine Moro, Pascal Wawa/Juuko Murshid dk46, Jonas Mkude/James Kotei dk46, Hassan Dilunga/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk76, Haruna Niyonzima, Hunlede Kissimbo/Meddie Kagere dk46, Emmanuel Okwi/Muzamil Yassin dk66 na Clatous Chama Afc leopards: Adira Jairus, Kipyegon Isaac/Mburu Moses dakika ya 85, Oduro Isaac, Kamura Robinson, Seda Edward, Marita Brian, Whyvonne Isuza, Mukangula Eugene/Ochuka Clark dk79, Wayyeka Tutawe/Vincent Oburu dk50, Okaka Aziz/Marita Brian na Odenyi Jaffar/Sikhayi Dennis dk75.
Mazraoui 'important' for Man United - Amorim
-
Ruben Amorim says Noussair Mazraoui's ability to play different positions
is important for Manchester United after he started at centre-back in the
new coa...
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
-
TP Mazembe have won the 2024 CAF Women’s Champions League title after they
defeated ASFAR 1-0 in the final on Saturday evening, played at the Ben
M’Hamed...
Edozie Njoku and the new APGA
-
By Ambrose Ododo it has been a long and tortuous journey for the birth of
the rebranded All Progressives Grand Alliance, APGA, and it looks like it
is go...
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment