// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MBEYA CITY YAKATAA KUMTOA KWA MKOPO AMBOKILE PAMOJA NA KUFUZU MISRI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MBEYA CITY YAKATAA KUMTOA KWA MKOPO AMBOKILE PAMOJA NA KUFUZU MISRI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, January 25, 2019

    MBEYA CITY YAKATAA KUMTOA KWA MKOPO AMBOKILE PAMOJA NA KUFUZU MISRI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMABULIAJI wa Mbeya City, Eliud Ambokile amerejea jana kutoka Misri alipokwenda kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.
    Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu kutoka Mbeya kwamba Ambokile amerejea baada ya kufanya vizuri katika majaribio yake katika klabu ya El Gounah.
    Hata hivyo, Kimbe amesema kwamba pamoja na Ambokile kufanya vizuri katika siku zake sita za majaribio, lakini hawajafikia makubaliano na El Gounah na kwamba dili hilo linaweza kuibuliwa tena Julai.

    Eliud Ambokile amerejeakutoka Misri alipokwenda kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa 

    “Hawa mabwana bada ya kumjairbu kwa siku sita, wakataka kumchukua kwa mkopo, au acheze kwanza kwa miezi sita ndiyo waaamue kumnunua moja kwa moja diirsha kubwa. Lakini sisi tukaona wao kuendelea kuwa naye bila kumnunua ni kuwaminyia nafasi wengine wanaomtaka,” amesema Kimbe na kuongeza;
    “Tukakubaliana tu arudi, aangale maeneo mengine huku akifanyia kazi mapungufu yake yaliyoonekana, kwa sababu kuna watu walionyesha nia mapema, lakini hawakuleta maombi, walikuwa wanasubiri msimu umalizike, ndiyo maana tumeona arudi kujaribu bahati kwingine,”amesema.
    Na Eliud amerudi wakati mwafaka, kwani Mbeya City wanakabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Mashujaa mjini Kigoma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAKATAA KUMTOA KWA MKOPO AMBOKILE PAMOJA NA KUFUZU MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top