Beki Mbrazil, David Luiz akishangilia baada ya kufunga penalti ya nne ya Chelsea kuipeleka Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup kufuatia ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Tottenham Hotspur jana Uwanja wa Stamford Bridge mjini London katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali. Chelsea ilishinda 2-1 na kufanya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza na mbali ya Luiz wengine waliofunga penalti za The Blues ni Willian, Azpilicueta na Jorginho, wakati Christian Eriksen na Erik Lamela pekee walifunga za Spurs, huku Eric Dier na Lucas Moura wakikosa. Chelsea itakutana na Manchester City katika fainali Februari 24 Uwanja wa Wembley mjini London PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Colts' Jonathan Taylor's 218 Yards, 3 TDs Wow NFL Fans Amid Fantasy
Football Playoffs
-
Indianapolis Colts star running back Jonathan Taylor had a monster day in
the team's win over the Tennessee Titans, and fantasy football managers who
have ...
47 minutes ago
0 comments:
Post a Comment