Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA SC itakutana na Nkana FC ya Zambia katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kushiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baadaye mwezi huu.
Hiyo ni baada ya Nkana FC kuifunga UD Songo ya Msumbiji 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Nkana mjini Kitwe, Zambia hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya kushinda 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Chiveve mjini Beira wiki iliyopita.
Nkana FC ni timu ambayo anachezea beki wa zamani wa Simba, Hassan Ramadhani Kessy aliyewahi pia kuchezea Mtibwa Sugar ya Morogoro na Yanga ya Dar ers Salaam.
Beki wa zamani wa Simba, Hassan Ramadhani Kessy akiichezea Nkana FC
Simba SC imefuzu kwa ushindi wa jumla wa 8-1 ikishinda 4-1 Dar es Salaam na 4-0 jana Manzini, mabao ya Clatous Chama mawili, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi.
Mechi ya kwanza itafanyika mjini Kitwe nchini Zambia kati ya Desemba 14 na 16 na marudiano yatakuwa Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kati ya Desemba 21 na 23.

0 comments:
Post a Comment