Na Alphonce Kabilondo, GEITA
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii John Costantine Kanyasu amelitaka shirika la hifadhi za Taifa nchini TANAPA kukitumia chama cha riadha nchini kutangaza vivutio vinavyo patikana kwenye hifadhi za Taifa pamoja na wanariadha wakubwa wa ndani na nje ya nchi wakimbiza beiskeli maarufu .
Naibu Waziri ametoa kauli hiyo Mjini Chato Mkoani Geita wakati akikabidhi zawadi mbali mbali vyeti pamoja na fedha kwa washindi wa riadha ,mbio za baiskeli walioshiriki bonaza la Rubondo Marathon lililokuwa limeandaliwa na hifadhi ya kisiwa cha Rubondo kwa ufadhili wa shirika la hifadhi za Taifa nchini TANAPA na shirika la Umeme Tanesco Wilayani Chato .
Kanyasu alisema kuwa shirika hilo halina budi kukitumia chama cha riadha nchini pamoja na wanariadha wakubwa , wakimbiza baiskeli maarufu wanaotambulika na kuwataka walioshinda kwenye bonaza la Rubondo Marathon kuwenda kuwa mabalozi wazuri wakukitangaza kisiwa cha hifadhi ya Rubondo pia amelitaka shirika hilo kuboresha bonaza hilo na kwamba lifanyike kila mwaka kwa kuzingatia sheria na kanuni za riadha na mbio za beiskeli kuepuka kupata washindi wasio stahili.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii John Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi Shamim Ramadhani mshindi wa mbio za kilometa kumi baada ya kuibuka mshindi kwenye bonaza la Rubondo Marathon
Aidha Masunga Duba aliyeibuka mshindi wa kwanza kwa wanaume kwenye mbio za beiskeli kutoka Mkoa wa Simiyu na hivyo kuibuka na kitita cha shilingi milioni moja akatumia kutoa kili chao kwa serikali kuwa iwawezeshe kupata baiskeli za kisasa zitakazo wawezesha kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na kuitanza Tanzania ambapo mshindi wa riadha kilometa kumi Shamim Ramadhani amesema kuwa mashindano hayo yaweendelevu ambapo amewashauri washiriki wenzake kutokata tama .
Mratibu wa bonaza hilo Alieth Ngaiza akitoa taarifa fupi kwa Naibu Waziri huyo amesema kuwa bonaza liliasisiwa na wasomi wa chuo kikuu wasio na ajira kikundi cha mahusiano ya jamii MAMAJA lengo likiwa ni kuhamasisha kurinda maliasili na hifadhi za Taifa pamoja na utalii wa ndani na kwamba bonaza limehusisha washiriki kutoka mikoa ya Simiyu ,Mwanza, Shinyanga ,Arusha na wenyeji Mkoa wa Geita .

0 comments:
Post a Comment