// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ITC YA CHIRWA YATUA AZAM FC LAKINI HATAWEZA KUCHEZA LEO DHIDI YA STAND UNITED CHAMAZI SABABU YA LESENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ITC YA CHIRWA YATUA AZAM FC LAKINI HATAWEZA KUCHEZA LEO DHIDI YA STAND UNITED CHAMAZI SABABU YA LESENI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, December 04, 2018

    ITC YA CHIRWA YATUA AZAM FC LAKINI HATAWEZA KUCHEZA LEO DHIDI YA STAND UNITED CHAMAZI SABABU YA LESENI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    USAJILI wa mshambuliaji mpya wa Azam FC, Obrey Chirwa, umekamilika asilimia 100 baada ya Chama cha Soka Misri (EFA) kuiachia Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa kuituma kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
    EFA imeachia ITC yake baada ya Nogoom FC kuithibitishia kuwa wameachana na mchezaji huyo na yupo huru kujiunga na timu yoyote, ambapo wiki chache zilizopita Azam FC ilimaliza taratibu za kumuhamisha kwa kuingia naye mkataba wa mwaka mmoja.
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Nurdin Amin ‘Popat’, amesema kwamba tayari kibali hicho kimeshatumwa TFF na sasa wanachosubiri ni kukamilika kwa vibali vyake vya kufanya kazi nchini pamoja na leseni itakayomwezesha kucheza soka nchini.
    “Tunamshukuru Mungu leo jioni (jana) TFF imetupa taarifa ya kupokea ITC ya Chirwa kutoka Misri alipokuwa akicheza awali, hataweza kuiwahi mechi ya leo kutokana na kutokuwa na leseni ya kucheza ligi na kibali chake cha kufanya kazi kutokamilika, tunatarajia atacheza mechi ijayo ya Ijumaa dhidi ya Mbao,” alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ITC YA CHIRWA YATUA AZAM FC LAKINI HATAWEZA KUCHEZA LEO DHIDI YA STAND UNITED CHAMAZI SABABU YA LESENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top