// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC YATOKA NYUMA NA KUITANDIKA STAND UNITED 3-1 CHAMAZI NA KUENDELEA KUIKARIBIA YANGA KILELENI LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC YATOKA NYUMA NA KUITANDIKA STAND UNITED 3-1 CHAMAZI NA KUENDELEA KUIKARIBIA YANGA KILELENI LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, December 04, 2018

    AZAM FC YATOKA NYUMA NA KUITANDIKA STAND UNITED 3-1 CHAMAZI NA KUENDELEA KUIKARIBIA YANGA KILELENI LIGI KUU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Azam FC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Stand United mabao 3-1 usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
    Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza timu hizo zikimaliza bila kufungana, kipindi cha pili Stand United walitangulia kwa bao la Hafidh Mussa dakika ya 53, kabla ya Azam FC kutokea nyuma na kuibuka na ushindi huo.
    Alianza kiungo Mghana, Enock Atta-Agyei kuisawazishia Azam FC dakika ya 66 kabla ya mshambuliaji chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Yahya Zayed kufunga mfululizo dakika ya 72 kwa penalti na 85.

    Yahya Zayed akishangilia baada ya kufunga mabao mawili leo dhidi ya Stand United

    Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 36 baada ya kucheza 14, ikiendelea kukamata nafasi ya pili nyuma ya Yanga SC, yenye pointi 38 za mechi 14 pia.
    Mabingwa watetezi, Simba SC wanafuatia katika nafasi ya tatu kwa pointi zao 27 za mechi 12 wakiwa na viporo viwili kutokana na kukabiliwa na mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YATOKA NYUMA NA KUITANDIKA STAND UNITED 3-1 CHAMAZI NA KUENDELEA KUIKARIBIA YANGA KILELENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top