Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Malangwe Mchungahela amesema kwamba hawamtambui Yussuf Manji kama Mwenyekiti wa Yanga.
Hayo yamekuja mara baada ya wajumbe wa kamati ya utendaji walipokutana na mwenyekiti huyo huku wakiwa na hoja ya kukubali kufanya uchaguzi isipokuwa nafasi ya uwenyekiti.
Mchungaha alisema kuwa kwa mujibu wa katiba ya Yanga, ibara ya 28 kanuni ya tatu (c) inasema mjumbe atakoma kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji iwapo atashindwa kutekeleza majukumu ya mjumbe kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa kipindi cha miezi 12 mfululizo.
TFF Imesema haItambui Uenyekiti wa Yussuf Manji Yanga SC na akitaka kuendelea kuwa kiongozi wa klabu hiyo agombee
Katiba hiyo ya marekebisho ya mwaka 2010, ibara ya 14 inamruhusu mwanachama yoyote kujiuzulu na kuwasilisha barua kwa katibu mkuu wa Yanga kwa barua ya rejesta.
Mchungahela alisema kuwa hawamtambui Manji kama mwenyekiti wa Yanga kama katiba yao inavyojieleza.
Alisema kuwa kama Manji bado anahitaji nafasi ya uenyekiti basi aende kuchukua fomu kabla mchakato haujafungwa aili aweze kugombea tena.
"Sisi kama TFF hatumtambui Manji kama mwenyekiti wa Yanga maana alishakutana na Waziri wa Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ili kuzungumzia suala la kurudi Yanga na alimkatalia.
Lakini pia aliandikiwa barua na TFF ambao walitaka kujua kama yeye bado mwenyekiti au la pia nayo alikaidi kujibu na alikuuja kujibu majibu ambayo hatoshelezi kujua kama yeye bado yupo kwenye nafasi yake," alisema Mchungahela.
Kwenye mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo waliokutana Juni 10 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Polisi, Oysterbay kwa pamoja walisema wanamtambua Manji kama mwenyekiti wao na wanamuamba amalizie miaka miwili iliyobaki kwakuwa muda wake unatarajiwa kumalizika Juni 2020.
Mei 23, mwaka jana Manji aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, akidai kuwa anatoa nafasi kwa wanachama wengine kuingoza klabu hiyo.
Kwa muda ambao Manji alitangaza kujiuzulu mpaka sasa kafikisha miezi 18 ambapo kapoteza sifa ya kuwa mwanachama hai wa klabu hiyo.
Mbali na Manji, wengine waliojiuzulu ni Clement Sanga (makamu mwenyekiti), Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi, Said Ameir na Hashim Abdallah (wajumbe).

0 comments:
Post a Comment