// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAONGEZA MUDA WA WANACHAMA WA YANGA SC KUCHUKUA FOMU ZA KUOMBA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA JANUARI 13 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAONGEZA MUDA WA WANACHAMA WA YANGA SC KUCHUKUA FOMU ZA KUOMBA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA JANUARI 13 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, November 15, 2018

    TFF YAONGEZA MUDA WA WANACHAMA WA YANGA SC KUCHUKUA FOMU ZA KUOMBA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA JANUARI 13

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesogeza mbele tarehe ya mwisho ya zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kugombea Uongozi katika Klabu ya Yanga SC.
    Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo alisema jana mjini Dar es Salaam kwamba zoezi hilo limeongezwa siku tano na sasa litakwenda hadi Novemba 19, 2018 ambapo awali zoezi lilikuwa linafikia tamati leo Novemba 14,2018.
    Wanachama tayari wameanza kujitokeza katika zoezi hilo la uchukuaji na urudishaji wa fomu.

    Aidha Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Young Africans zinatarajia kukutana Ijumaa Novemba 16,2018
    Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Januari 13, 2019 nafasi zinazogombewa zikiwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
    Hadi sasa waliochukua fomu ni Yono Kevela na Dk. Jonas Tiboroha wanaowania Uenyekiti, Dominick Francis, Said Baraka, Pindu Luhoyo, Shaffi Amri, Mussa Katabaro, Salim Seif, Sylvestre Haule, Benjamin Mwakasonda na Hamad Ali Islam wanaowania Ujumbe.  

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAONGEZA MUDA WA WANACHAMA WA YANGA SC KUCHUKUA FOMU ZA KUOMBA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA JANUARI 13 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top