Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
BAADA ya rais John Pombe Magufuli kutoa agizo kwa timu za Tanzania kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika, Simba inayoshiriki Ligi ya Mabingwa imeonesha dhamira yake ya kufanya vizuri kwenye mashindano hiyo.
Simba watashuka dimbani Novemba 28 kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mabingwa wa eSwatini, zamani Swaziland, Mbabawe Swallows kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa timu ya Simba Hajji Manara alisema kuwa wamepewa maagizo na Rais Magufuli kuhakikisha wanakuwa mabingwa wa Afrika kwenye michuano hiyo na watahakikisha wanafanya vizuri.
Amesema kuwa wanaajua ugumu wa kupata ubingwa kwenye Afrika lakini wanadhamira na dhamira yao ya kwanza ni kuhakikisha wanaingia kwenye hatua za makundi kwenye mashindano hayo.
Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli anataka timu za Tanzania zifanye vizuri kwenye mashindano ya kimataifa
Alisema kuwa kama Mungu akiwajaalia wakaingia kwenye hatua hiyo ya makundi lolote linaweza kutokea kuanzia hapo.
"Tukifanikiwa kufuzu kuingia kwenye hatua za makundi basi tunaweza kufika popote, tuajua haitakuwa rahisi lakini tutahakikisha tunapambana ili tufike mbali zaidi," Alisema Manara
Manara alisema kuwa Mbabawe Swallows, siyo timu rahisi ya kuibeza na ndio maana tunajipanga ili kuhakikisha tunashinda mchezo huo.
Amesema kuwa watahakikisha wanautumia vyema uwanja wa nyumbani kwa kupata ushindi mnono ili wakienda kwenye mchezo wa marudiano wawe na rekodi nzuri.
Hata hivyo Manara amesema kuwa kikosi chao kinatarajiwa kushuka dimbani Novemba 16, Ijumaa kuvaana na mabingwa wa Malawi, Big Bullets, kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni.
Manara alisema kiingilio katika mchezo huo kitakuwa sh. 3,000, sh. 7,000 na sh. 10,000, aliwaomba mashabiki wa Simba kumwagika kwa wingi uwanjani hapo kuishangilia timu yao.
"Mchezo wetu huu na wa Ligi dhidi ya Lipuli FC tutakaocheza Novemba 21, tutautumia vyema kama sehemu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbabane, tunaamini mwalimu atayafanyia kazi mapungufu atakayoyaona kwenye mchezo huo kabla ya kukutana na mabingwa hao wa Swaziland," alisema.
Ni miaka saba tangu Simba irejee tena kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mara ya mwisho walishiriki mwaka 2003, walipofanikiwa kufika hatua ya makundi ya michuano ya kimataifa baada ya hapo wakapotea kabla ya kutwaa ubingwa msimu uliopita.
Swallows kwao ni mara ya pili mfululizo kushiriki michuano hii ambapo msimu uliopita waliishia hatua ya makundi sasa wamerejea tena kwenye michuano hiyo.
Simba walichukua Ubingwa baada ya kucheza michezo 30 wakiwa na Pointi 69 baada ya kutoa sare michezo tisa na kupoteza mchezo mmoja huku wakishinda michezo 20.
Kama Simba watapita hatua hiyo ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, raundi ya kwanza watakutana na mshindi kati ya Nkana Rangers ya Zambia dhidi ya Uniao Desportiva Do Songo ya Mozambique.

0 comments:
Post a Comment