Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MABINGWA wa kihistoria wa Tanzania, Yanga SC juzi walikuwa wana mchezo wa kirafiki visiwani Zanzibar na wakaibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malindi FC Uwanja wa Amaan.
Nyota wa mchezo wa huo alikuwa mkongwe, kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa aliyefunga bao moja na kuseti moja katika ushindi huo.
Ngassa anayecheza Yanga kwa mara ya tatu baada ya kurejea tena msimu huu, alimtilia krosi nzuri Emmanuel Martin kufunga bao la kwanza dakika ya 43 kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 60 akimalizia krosi ya Pius Buswita.
Mchezo wa leo ulikuwa maalum kumuaga aliyekuwa Nahodha wake na beki hodari, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliyestaafu Mei mwaka huu.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Mzambia Noel Mwandila alibadili karibu kikosi chote baada ya bao la pili, lakini langoni kijana Ramadhani Awam Kabwili alimaliza dakika zote 90.
Na kwake ikawa mechi ya 16 ya mashindano tangu amesajiliwa Yanga SC Januari mwaka huu kama kipa wa tatu, kufuatia kufanya vizuri akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
Katika mechi hizo 16 ambazo Kabwili aliyeibukia akademi ya Azam FC ameidakia Yanga SC, aliweza kusimama langoni kwenye michezo 10 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.
Na hata mechi sita alizoruhusu mabao, inaonekana kabisa ilitokana na uchanga wake tu, lakini kadiri siku zinavyokwenda mbele atakuwa kipa mgumu mno kufungika.
Kabwili ambaye Desemba 11, atafikisha miaka 18, alikuwa kipa namba moja wa Serengeti Boys kwenye Fainali za U17 Afrika Mei mwaka jana nchini Gabon ambako alidaka kwa ustadi mkubwa kiasi cha kuwa gumzo huko.
Haikuwa ajabu mwaka huu alipopandishwa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes na kuanza kuitwa timu ya wakubwa, Taifa Stars kupata uzoefu.
Kabwili anahitaji kufanya bidii zaidi katika mazoezi na kuwa na malengo ya kufika mbali ili aingie kwenye orodha ya makipa bora wa kihistoria wa nchi, kwani kipaji tayari anacho.
Unaweza kusemaje juu ya mlinda mlango huyo chipukizi, akiwa ana umri wa 17 na ushei tu anadakia timu ya Ligi Kuu mechi 10 bila kuruhusu bao kati ya 16 tu kama si kumtabiria kuwa tegemeo la klabu yake na nchi baadaye?
REKODI YA RAMADHANI KABWILI YANGA SC
1. Yanga 0-1 Ruvu Shooting (Alifungwa moja kirafiki - Chamazi)
2. Yanga 2-0 Mlandege (Hakufungwa Kirafiki Zanzibar)
3. Yanga 1-0 Chipukizi (Aliingia kipindi cha pili kirafiki Zanzibar)
4. Yanga 0-0 KMC (Hakufungwa Kirafiki Chamazi)
5. Yanga 0-0 Rhino Rangers (Aliingia dk83 hakufungwa Kirafiki Ally Hassan Mwinyi)
6. Yanga 2-1 Mlandege (Alifungwa moja Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
7. Yanga 2-0 Taifa Jang’ombe (Hakufungwa Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
8. Yanga SC 1-0 Zimamoto( Hakufungwa Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
9. Yanga 2-0 Lipuli FC (Hakufungwa, aliingia dk17 baada ya Youthe Rostand kuumia, Samora, Iringa)
10. Yanga 4-0 Njombe Mji FC (Hakufungwa Ligi Kuu, Samora, Uhuru)
11. Yanga 1-0 Saint Louis FC (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa, Taifa)
12. Yanga 4-1 Maji Maji FC (alifungwa moja kwa penalti, Ligi Kuu, Taifa)
13. Yanga 1-2 Township Rollers (Alifungwa mbili Ligi ya Mabingwa Taifa)
14. Yanga 2-2 Ruvu Shooting FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Taifa)
15. Yanga 1-3 Azam FC (Alifungwa tatu Ligi Kuu Taifa)
16. Yanga SC 2-0 Malindi FC (Hakufungwa Kirafiki Zanzibar).

Ramadhani Kabwili (kulia) akiwa na Kocha Msaidizi wa Azam FC, Iddi Nassor 'Cheche' ambaye alikuwa kocha wake Azam Akademi. Hii ilikuwa baada ya mechi ya Yanga na Azam Ligi Kuu msimu huu |
REKODI YA RAMADHANI KABWILI YANGA SC
1. Yanga 0-1 Ruvu Shooting (Alifungwa moja kirafiki - Chamazi)
2. Yanga 2-0 Mlandege (Hakufungwa Kirafiki Zanzibar)
3. Yanga 1-0 Chipukizi (Aliingia kipindi cha pili kirafiki Zanzibar)
4. Yanga 0-0 KMC (Hakufungwa Kirafiki Chamazi)
5. Yanga 0-0 Rhino Rangers (Aliingia dk83 hakufungwa Kirafiki Ally Hassan Mwinyi)
6. Yanga 2-1 Mlandege (Alifungwa moja Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
7. Yanga 2-0 Taifa Jang’ombe (Hakufungwa Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
8. Yanga SC 1-0 Zimamoto( Hakufungwa Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
9. Yanga 2-0 Lipuli FC (Hakufungwa, aliingia dk17 baada ya Youthe Rostand kuumia, Samora, Iringa)
10. Yanga 4-0 Njombe Mji FC (Hakufungwa Ligi Kuu, Samora, Uhuru)
11. Yanga 1-0 Saint Louis FC (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa, Taifa)
12. Yanga 4-1 Maji Maji FC (alifungwa moja kwa penalti, Ligi Kuu, Taifa)
13. Yanga 1-2 Township Rollers (Alifungwa mbili Ligi ya Mabingwa Taifa)
14. Yanga 2-2 Ruvu Shooting FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Taifa)
15. Yanga 1-3 Azam FC (Alifungwa tatu Ligi Kuu Taifa)
16. Yanga SC 2-0 Malindi FC (Hakufungwa Kirafiki Zanzibar).
0 comments:
Post a Comment