TIMU ya taifa ya Uganda, The Cranes imejiimarisha kileleni mwa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Lesotho jioni ya leo Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, Uganda.
Kwa ushindi huo, Uganda inafikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, ikishinda mbili na kutoa sare, sasa ikifuatiwa na Cape Verde pointi nne za mechi tatu pia, wakati Tanzania yenye pointi mbili sawa na Lesotho ni ya tatu kwa wastani wa mabao.
Ushindi wa leo wa The Cranes umetokana na mabao ya washambuliaji wake, Emmanuel Okwi anayechezea klabu ya Simba ya Tanzania aliyefunga mawili dakika za 11 na 63 na Faruku Miya wa Farouk Miya wa HNK Gorica ya Croatia kwa penalti dakika ya 36.
Emmanuel Okwi (katikati) akishangilia na Faruku Miya (kulia) baada ya wote kufunga leo
Timu hizo zitarudiana Jumanne Uwanja wa Setsoto mjini Maseru, siku ambayo Cape Verde watakuwa wanarudiana na Tanzania Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam baada ya ushindi wa 3-0 jana nyumbani Uwanja wa Taifa mjini Praia.

0 comments:
Post a Comment