// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MWASISI WA TUKUYU STARS RAMNIK PATEL ‘KAKA’ AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO MJINI MBEYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MWASISI WA TUKUYU STARS RAMNIK PATEL ‘KAKA’ AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO MJINI MBEYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, October 18, 2018

    MWASISI WA TUKUYU STARS RAMNIK PATEL ‘KAKA’ AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO MJINI MBEYA

    Na Mwandishi Wetu, MBEYA
    MWASISI wa klabu ya Tukuyu Stars, Ramnik Patel ‘Kaka’ amefariki dunia alfajiri ya leo, nyumbani kwao Uhindini mkoani Mbeya. 
    Patel amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, kiasi cha kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya Jiji la Mbeya tangu Agosti mwaka huu.
    Patel ndiye mwanzilishi wa timu hiyo na alifanikiwa kuipandisha daraja na kuchukua ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1986.
    Hata hivyo, msimu wa 1987 iliteremka Daraja na Kaka akahangaika nayo hadi kuipandisha tena msimu wa 1988 alipoirejesha Ligi Kuu na kuikabidhi kwa Halmshauri ya Wilaya ya Tukuyu, ambako huko ndipo ilipofia.

    Ramnik Patel ‘Kaka’ alipokuw aamelazwa hospitali ya Mbeya kabla kufariki dunia leo 

    Lakini Tukuyu inakumbukwa kwa kuibua vipaji vya nyota wengi wa soka mara zote, kuanzia akina Salum Kabunda ‘Ninja’, Justin Mtekere (wote marehemu), Godwin Aswile ‘Scania’ na baadaye akina Stephen Mussa (sasa marehemu) na Sekolojo Chambua.   
    Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ramnik Patel ‘Kaka’, Mbeya na Tanzania nzima itakukumbuka kwa mchango wako kwenye michezio enzi za uhai wako. Amin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWASISI WA TUKUYU STARS RAMNIK PATEL ‘KAKA’ AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO MJINI MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top