MASHABIKI wa Leicester City ya England wapo katika majonzi baada ya taarifa kwamba mmiliki wa klabu yao, Vichai Srivaddhanaprabha alikuwemo kwenye Helikopta iliyoteketea kwa moto baada ya kulipuka na kuungua nje ya Uwanja wa King Power mjini Leicester, Leicestershire jana.
Tukio hilo lilitokea dakika chache tu baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya England jana, Leicester City wakilazimishwa sare ya kufungana bao na 1-1 West Ham, wageni wakitangulia kwa bao la Fabian Balbuena dakika ya 30 kabla ya Wilfred Ndidi kuwasawazishia wenyeji, dakika ya 89.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema kwamba waliona helikopta hiyo inaungua muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka uwanjani hapo.
BBC imeripoti mmiliki wa Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha alikuwepo kwenye helikopta iliyoteketea kwa moto jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Lakini chanzo cha kulipuka kwa helikopta hiyo inaelezwa na hitilafu za kwenye injini.
Inadaiwa mmiliki wa Leicester, Vichai Srivaddhanaprabha - pamoja na watu wengine wawili walikuwepo kwenye hilokopta hiyo wakati inateketea kwa moto.
Taarifa za awali zilisema kwamba binti ya Srivaddhanaprabha alikuwepo kwenye helikopta hiyo wakati inateketea moto, ingawa Leicester FC wamekanusha madai hayo.
Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC) limeripoti kwamba chanzo kutoka kwenye familia mmiliki huyo wa Leicester alikuwepo kwenye helikopta hiyo.
Mashabiki walishitushwa mno na tukio hilo na wengine waliangulia vya machozi baada ya ndege hiyo kuingizwa ndani ya Uwanja kwenye eneo la kuegeshea magari.
Srivaddhanaprabha alikuwa mchora ramani wa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England walilochukua Leicester katika msimu ambao walipanda kutoka Daraja la Kwanza, mwaka 2016.
Aliibadilisha kabisa klabu hiyo baada ya kuinunua mwaka 2016 kwa dau la Pauni Milioni 39 mwaka 2010.

0 comments:
Post a Comment