Na Mwandishi Wetu, DARES SALAAM
TIMU ya Azam FC imepoteza mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam baada ya kufungwa 2-1 na Transir Camp ya Daraja la Kwanza.
Azam FC iliyocheza bila sehemu kubwa ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza waliokwenda kujiunga na timu zao mbalimbali za taifa, ilionyesha mchezo mzuri lakini ikazidi maarifa kidogo tu na Camp.
Transit Camp inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ilionyesha mabadiliko makubwa kikosini mwake kutoka msimu uliopita, ikirejea na vijana wengi wapya na wadogo.
Baada ya mchezo wa leo dhidi ya Transit Camp inayojipanga kurejea Ligi Kuu, Azam FC watateremka tena uwanjani Jumanne jioni kumenyana na Arusha United katika mchezo mwingine wa kirafiki.
Kocha Mholanzi wa Azam FC, Hans van der Pluijm anataka kutumia wiki hii ya mapumziko ya kupisha kalenda ya mechi za kimataifa kuwa kuwajengea uzoefu wa mechi wachezaji wake wa akiba.

0 comments:
Post a Comment