Na Lulu Ringo, DAR ES SALAAM
KUMEKUWA na maswali mengi kwa mashabiki mbalimbali wa soka baada ya kuona mshambuliaji wa Coastal Union, Ali Kiba haonekani uwanjani akiichezea timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Bara tangu asajiliwe mwanzoni mwa msimu huu.
Wengi wamekuwa wakisubiri mechi kubwa ambazo ni Coastal Union dhidi ya Yanga au Simba wakiamini labda umaarufu wa mchezaji huyo utafanya mchezo uwe na morali kubwa kutokana na wingi wa mashabiki wa timu zote mbili ambao pia ni mashabiki wa mchezaji huyo.
Jana kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union ilicheza na Yanga lakini Ali Kiba hakucheza japokuwa alionekana uwanjani akipasha misuli moto na wachezaji wenzake.
Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda alipoulizwa sababu za Ali Kiba kutocheza, alisema wakati ukifika mchezaji huyo ataitumikia timu yake.
Juma Mgunda (kulia), kocha wa Coastal Union akiwa na wasaidizi wake
“Naomba hili niliweke wazi, Ali Kiba ni mchezaji wa Coastal Union, amesajiliwa na ni mtumishi wa Coastal Union, ukifika wakati wa kuitumikia timu ataitumika na wala hilo halina wasiwasi,” alisema
Mgunda.
Aidha, Mgunda amesema ameridhika na kiwango cha wachezaji wake kilichoonyeshwa jana katika mchezo wao dhidi yaYanga atakua hajawatendea haki.
“Nisiporidhika na kiwango walichoonyesha wachezaji wangu nitakua sijawatendea haki, nimeridhika na kiwango chao na nina imani kadiri tunavyoendelea tutafanya vizuri,” alisema kocha huyo.
Coastal Union walipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga, bao lililofungwa dakika ya 11 na Harieter Makambo akiwa amepokea pasi ya Ibrahim Ajib.

0 comments:
Post a Comment