// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LIPULI FC YAENDA MECHI YA TATU MFULULIZO BILA USHINDI LIGI KUU, YATOKA 0-0 NA MTIBWA SAMORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LIPULI FC YAENDA MECHI YA TATU MFULULIZO BILA USHINDI LIGI KUU, YATOKA 0-0 NA MTIBWA SAMORA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, September 15, 2018

    LIPULI FC YAENDA MECHI YA TATU MFULULIZO BILA USHINDI LIGI KUU, YATOKA 0-0 NA MTIBWA SAMORA

    Na Mwandishi Wetu, IRINGA
    TIMU ya Mtibwa Sugar imelazimishwa sare ya bila kufungana na wenyeji, Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Samora mjini Iringa.
    Hiyo ni sare ya kwanza kwa Mtibwa Sugar, inayofundishwa na kocha Zubery Katwila baada ya kushinda mechi mbili nyumbani na kufungwa moja ugenini katika tatu za awali.
    Kwa Lipuli FC ya kocha Suleiman Matola, hiyo ni sare ya tatu mfululizo baada ya sare mbili za awali zote 1-1 na ugenini dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na JKT Tanzania Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni.

    Mshambuliaji wa Lipuli FC, Paul Nonga akifumua shuti mbele ya beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Daudi

    Mchezo wa leo ulikuwa ni wa mashambulizi ya pande zote mbili na kila timu ilicheza vizuri, lakini tu safu za ulinzi zilikuwa imara zaidi.
    Sasa Mtibwa Sugar inafikisha pointi saba katika mechi ya nne kuelekea mchezo wake ujao na Ndanda FC mjini Mtwara Jumatano, wakati Lipuli inafikisha pointi tatu kuelekea mechi yake ijayo na AllianceFC Jumatano hapo hapo Iringa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIPULI FC YAENDA MECHI YA TATU MFULULIZO BILA USHINDI LIGI KUU, YATOKA 0-0 NA MTIBWA SAMORA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top