Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba SC ya Dar es Salaam imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na Kampuni ya A1 Products kupitia kinywaji cha Mo Energy Drink wenye thamani ya Sh. Milioni 250.Hiyo ni moja ya makampuni yanayomilikiwa na mmiliki mtarajiwa wa klabu hiyo, Mohammed ‘Mo’ Dewji kupitia kampuni yake mama, Mohamed Enterprises Limited (MeTL)
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Kaimu Rais Simba SC, Salim Abdallah 'Try Again' amesema fedha zote za udhamini huo zitaenda katika mradi wa ujezi wa Uwanja mpya wa klabu huko Bunju.
Pamoja hayo, Simba SC leo imezindua jezi zake mpya za msimu ujao kwa ajili ya mashabiki wake ambazo zitakuwa zinauzwa kwa Sh. 25,000.
Simba SC imefanya yote hayo saa chache tu baada ya kurejea mjini Dar es Salaam leo Alfajiri kutoka nchini Uturuki ambako ilikwenda kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya.
Pamoja na mazoezi, ziara hiyo ilihusisha mechi mbili za kujipima nguvu kwanza sare ya 1-1 na MC Oujder ya Morocco na nyingine ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi F.C.E Ksaifa ya.
Katika sare ya 1-1 bao la Simba SC lilifungwa na Adam Salamba na kwenye ushindi wa 3-1 mabao ya Wekundu hao yalifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi mawili na lingine Mnyarwanda, Meddie Kagere.
Mabingwa hao wa Tanzania wanatarajiwa kumenyana na mabingwa mara mbili wa Afrika, Asante Kotoko ya Ghana Jumatano Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
0 comments:
Post a Comment