KIPA Hugo Lloris anaweza kupoteza Unahodha wa Tottenham pamoja na kushinda Kombe la Dunia, kufuatia kukamtwa Saa 8.20 usiku akiwa anaendesha gari amelewa katikati ya London jana na kufunguliwa mashitaka ya kuendesha akiwa amelewa kupita kiasi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa Nahodha wa kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia mwezi uliopita nchini Urusi, alikamatwa na Polisi Gloucester Place, jirani na Mtaa wa Baker akiwa amelewa chakari.
Nyota huyo wa Spurs alikuwa ametoka na wachezaji wenzake wa Ufaransa, Laurent Koscielny wa Arsenal na mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud jioni kwenda Bagatelle huko Mayfair, ambayo ni mgahawa na sehemu ya ‘vinywaji vikali’.
Hugo Lloris anaweza kupoteza Unahodha wa Tottenham baada ya kukamtwa usiku wa manane akiwa anaendesha gari amelewa chakari PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Baada ya kukamatwa akiwa amelewa, Lloris, ambaye analipwa Pauni 150,000 kwa wiki, alipelekwa kituo cha Polisi cha Charing Cross ambako inaamini aliwekwa ndani kwa saa saba kabla ya kufunguliwa mashitaka na kuruhusiwa huku akitakiwa kufika Mahakama ya Westminster Magistrates mwezi ujao.
Inafahamika Tottenham imekasirishwa na kitendo cha Nahodha wake huyo kwenda kulewa huku wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United Jumatatu kiasi cha Lloris kurejea nyumbani Saa 5 asubuhi na kuchelewa mazoezini.

0 comments:
Post a Comment