// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KWA MWEZI MMOJA TU, WANAYANGA WAICHANGIA TIMU YAO SH. MILIONI 30 KARIBU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KWA MWEZI MMOJA TU, WANAYANGA WAICHANGIA TIMU YAO SH. MILIONI 30 KARIBU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, August 31, 2018

    KWA MWEZI MMOJA TU, WANAYANGA WAICHANGIA TIMU YAO SH. MILIONI 30 KARIBU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    JUMLA ya Sh 29,316,092 zimepatika kutokana na michango ya wapenzi na wanachama wa Yanga kwa klabu yao katika mwezi wa kwanza tu wa kampeni za kuchangia timu yao pendwa.
    Taarifa ya Yanga SC imesema kwamba hesabu za Agosti zimefungwa na kampeni za kuichangia klabu zimezalisha Sh. Milioni 29. 
    “Ahsante kwa sapoti, ahsante kwa kuchagua kuwa sehemu ya mafanikio, endelea kuchangia sasa kwa maendeleo ya timu yako,”imesema taarifa ya Yanga.
    Azam TV na Uhai Radio wanaendesha kampeni za kuwahamasisha wapenzi wa Yanga SC kuichangia klabu yao ambayo kwa sasa inakabiliwa na hali mbaya kifedha.
    Hiyo ni baada ya kumpoteza aliyekuwa Mwenyekiti wake, Yussuf Manji aliyekuwa mfadhili pia ambaye alijiuzulu Mei mwaka jana.
    Katikati ya mwaka huu wanachama walipinga ombi la Manji kujiuzulu katika mkutano uliofanyika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay mjini Dar es Salaam.
    Na Agosti 19 akaibuka Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam wakati wa mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger na pamoja na kuzunguka Uwanja kusabahi mashabiki, kuzungumza na wachezaji kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hakusema kama anarejea madarakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KWA MWEZI MMOJA TU, WANAYANGA WAICHANGIA TIMU YAO SH. MILIONI 30 KARIBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top