// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AKINA MSUVA WALAZIMISHA SARE NA MAZEMBE LUBUMBASHI, LAKINI WATOLEWA LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AKINA MSUVA WALAZIMISHA SARE NA MAZEMBE LUBUMBASHI, LAKINI WATOLEWA LIGI YA MABINGWA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, August 28, 2018

    AKINA MSUVA WALAZIMISHA SARE NA MAZEMBE LUBUMBASHI, LAKINI WATOLEWA LIGI YA MABINGWA

    Na Mwandishi Wetu, LUBUMBASHI
    WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva ametoa pasi ya bao la kusawazisha dakika ya mwisho, timu yake, Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco ikilazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, TP Mazembe katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
    Mazembe walitangulia kwa bao la penalti dakika ya 87 lililofungwa na mshambuliaji Mkongo, Ben Malango kabla ya kiungo Mmorocoo, Houssine Khoukhouche kuisawazishia Jadidi dakika ya 90 na ushei kwa pasi ys Msuva.
    Sare hiyo katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo, inamaanisha Jadidi inayomaliza na pointi sita inaaga michuano hiyo baada ya kuzidiwa kete na Mazembe iliyomaliza na pointi 12, ikifuatiwa ES Setif ya Algeria yenye pointi nane.
    Safari ya Simon Msuva Ligi ya Mabingwa Afrika 2018 imeishia hatua ya makundi baada ya kuzidiwa kete na Mazembe na ES Setif katika Kundi B

    Timu nyingine katika kundi hilo ni MC Alger ya Algeria pia iliyomalizia mkiani nayo kwa pointi zake tano wakiziacha Mazembe na Setif zikienda Nusu Fainali. 
    Msuva ameuanza msimu wake wa pili Difaa Hassan El-Jadidi aliyojiunga nayo kutoka Yanga SC ya nyumbani Tanzania Julai mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AKINA MSUVA WALAZIMISHA SARE NA MAZEMBE LUBUMBASHI, LAKINI WATOLEWA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top