BONDIA Deontay Wilder amesema kwamba wamekubaliana na Anthony Joshua kupigana mwezi Septemba au Oktoba nchini Uingereza.
Mmarekani huyo, anayeshikilia taji la WBC uzito wa juu, ametumia chaneli yake za mtandaoni kusema kwamba amekubali ofa ya vipengele vilivyotolewa na kambi ya Joshua kwa ajili ya pambano hilo la kuunganisha mataji.
Wilder anasema hayo siku chache tu baada ya promota wa Joshua, Eddie Hearn kusema kwamba hisia zake kubwa ni bondia wake huyo Muingereza anayeshikilia mataji ya IBF, WBO na WBA apigane na mshindani wa taji la WBA, Alexander Povetkin mwezi September, na pambano dhidi ya Wilder lifuatie kati ya Februari au Machi.
Deontay Wilder amesema wamekubaliana na Anthony Joshua kupigana mwezi Septemba au Oktoba Uingereza PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Hearn amekuwa kwenye majadiliano na wote, timu za Wilder na Povetkin juu ya pambano lijalo na wakati wote Wilder umekuwa mpango wa kwanza.
Mpinzani haswa ajaye wa Joshua bado ni kitendawili, hivuyo tuendelee kusubiri kama tamko la Wilder linaweza kuwa jibu sahihi.
Awali Wilder alitaka Joshua aende Marekani kwa pambano hilo kwa ofa ya dola za Kimarekani Milioni 50, lakini mpinzani wake huyo naye na Hearn wakashikilia msimamo wa pambano kufanyika Uingereza.
Wilder amesema jana usiku kwamba: "Pauni Milioni 50 kwa Joshua kupigana na mimi Marekani zipo pale pale kwa ajili yake kama nataka,".
0 comments:
Post a Comment