// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WASOMALI KUCHEZESHA MECHI YA YANGA NA GOR MAHIA KOMBE LA SHIRIKISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WASOMALI KUCHEZESHA MECHI YA YANGA NA GOR MAHIA KOMBE LA SHIRIKISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, June 13, 2018

    WASOMALI KUCHEZESHA MECHI YA YANGA NA GOR MAHIA KOMBE LA SHIRIKISHO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetaja waamuzi kutoka nchini Somalia kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi kati ya Gor Mahia ya Kenya na Young Africans ya Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Moi Kasarani Julai 18,2018.
    Kwenye mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Hassan Mohamed Hagi akisaidiwa na Mwamuzi namba 1 Hamza Hagi Abdi, Mwamuzi msaidizi namba 2 Suleiman Bashir Sh.Abdi na Mwamuzi wa akiba Nur Muhidin Mohamed.
    Mtathmini waamuzi anatokea Gabon Jan Olivier Mbera na Kamishna wa mchezo anatokea Africa Kusini Simphiwe Brian Xaba sambamba na mratibu wa mchezo huo Nomsa Jacobeth Mahlangu.

    Aidha mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa July 29,2018 Kwenye Uwanja wa Taifa wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Mauritius. 
    Mwamuzi wa katikati atakuwa Ahmed Imtehaz Heeralall akisaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Cauvelet Louis Ralph Fabian,Mwamuzi msaidizi namba 2 Akhtar Nawaz Rossaye na Mwamuzi wa akiba Ganesh Chutooree.
    Kamishna wa mchezo anatokea Zambia Patrick Kangwa, Mtathmini waamuzi anatokea Congo Louzaye Rene Daniel wakati Mratibu anatokea Nigeria Nasiru Sarkintudu Jibril.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WASOMALI KUCHEZESHA MECHI YA YANGA NA GOR MAHIA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top