// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SALAH AAHIDI KUIBEBA MISRI KOMBE LA DUNIA KUANZIA MWANZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SALAH AAHIDI KUIBEBA MISRI KOMBE LA DUNIA KUANZIA MWANZO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, June 09, 2018

    SALAH AAHIDI KUIBEBA MISRI KOMBE LA DUNIA KUANZIA MWANZO

    MSHAMBULIAJI Mohamed Salah amesema kwamba atakuwa fiti na tayari kuichezea Misri tangu mwanzo katika Kombe la Dunia Ijumaa ijayo.
    Mkali huyo wa mabao wa Liverpool, ambaye alikuwa nje kwa maumivu ya bega aliyoyapata katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid, ameyasema hayo leo wakati wa kuagwa na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi.
    Kulikuwa na wasiwasi kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kuikosa mechi ya kwanza ya Misri ya michuano hiyo ndani ya miaka 18, bada ya kuumia bega mjini Kiev.

    Mohamed Salah akisalimiana na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi wakati wa kuagwa leo kwa safari ya Misri kwenye Kombe la Dunia 

    MECHI ZA MISRI KUNDI A KOMBE LA DUNIA 

    Uruguay - Juni 16 - Saa 7.00 usiku
    Urusi - Juni 19 - Saa 1.00 usiku
    Saudi Arabia - Juni 25 - Saa 9.00 Alasiri
    Akizungumza katika hafla ya kuagwa kwa kikosi cha Misri kwenda Urusi kwenye Kombe la Dunia, Salah alikuwa mwenye kujiamini kwamba atakuwa tayari kwa mechi ya ufunguzi dhidi ya Uruguay Ijumaa ijayo mjini Yekaterinburg.
    "Nakuahidi, nitajitahidi kwa uwezo wangu kuwa tayari kwa Kombe la Dunia na kutimiza ndoto ya Misri," amesema mshambuliaji huyo akimuambia El-Sisi.
    "Najisikia vizuri sana sasa na nitakuwa tayari kucheza dhidi ya Uruguay. "Sitakata tamaa katika ndoto zetu. Naahidi kufanya kadiri ya uwezo wangu kwa ajili ya watu wetu,".' 
    Baada ya mechi yao ya ufunguzi ya Kundi A dhidi ya timu ya akina Luis Suarez, Misri watamenyana na wenyeji wa mashindano, Urusi Juni 19 kabla ya kumaliza na hatua ya kwanza kwa kumenyana na Saudi Arabia Juni 25.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SALAH AAHIDI KUIBEBA MISRI KOMBE LA DUNIA KUANZIA MWANZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top