// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RASMI, NCHIMBI NI MSHAMBULIAJI MPYA WA AZAM FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RASMI, NCHIMBI NI MSHAMBULIAJI MPYA WA AZAM FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, June 12, 2018

    RASMI, NCHIMBI NI MSHAMBULIAJI MPYA WA AZAM FC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Azam FC, imethibitisha kuingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji Ditram Nchimbi, akitokea Njombe Mji iliyoshuka Daraja.
    Nchimbi ni mmoja ya washambuliaji wachache kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambao wanatambulika kwa uwezo wa kupambana na mabeki kwa mipira ya juu na chini, akitarajiwa kuongeza kitu katika eneo la ushambuliaji la Azam FC.
    Zoezi la uingiaji mkataba baina ya pande hizo mbili limesimamiwa na Meneja wa timu hiyo, Phillip Alando, ambaye ameweka wazi kuwa ujio wa mshambuliaji huyo ni katika kuboresha eneo la ushambuliaji.

    Ditram Nchimbi (kulia) akisaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Azam FC kutoka Njombe Mji FC iliyoshuka. Kushoto ni Meneja wa klabu, Philipo Alando

    Mshambuliaji huyo aliyeipandisha Majimaji miaka mitatu iliyopita kwa mabao yake 10, amewahi pia kuichezea Mbeya City, ataanza kuonekana rasmi Azam FC kuanzia msimu ujao wakati timu hiyo ikianza kutetea ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagame inayotarajia kutimua vumbi kuanzia Juni 29 hadi Julai 13 mwaka huu.
    Huo ni usajili wa tatu kwa Azam FC kuelekea msimu ujao, awali ikitangulia kuwasajili nyota wawili kutoka Zimbabwe mshambuliaji Donald Ngoma na kiungo Tafadzwa Kutinyu, wote wakipendekezwa na Kocha Mkuu mpya, Hans Van Der Pluijm.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RASMI, NCHIMBI NI MSHAMBULIAJI MPYA WA AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top