CHIPUKIZI Justin Kluivert ametupilia mbali nafasi ya kucheza Ligi Kuu ya England baada ya kujiunga na Roma.
Kluivert, ambaye alikuwa anahusishwa na mpango wa kuhamia Manchester United, ameondoka Ajax kujiunga na Roma iliyofika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita kwa dau la Pauni Milioni 15.85.
Mchezaji huyo mweye umri wa miaka 19 alipokewa na mashabiki 500 wa Roma alipokuwa akiwasili Uwanja wa Ndege wa Fiumicino Airport jana jioni, kabla ya klabu kutangaza ujo wake kwenye ukura wao wa Twitter.
Justin Kluivert ametupilia mbali nafasi ya kucheza Ligi Kuu ya England baada ya kujiunga na Roma PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Atakamilisha vipimo vya afya wenye viwanja vya mazoezi vya Roma leo kabla ya kutambulishwa rasmi leo Uwanja wa Olimpico.
Kluivert, ambaye mi mmoja wa watoto watatu wa kiume wa gwiji wa Ajax, Patrick, amekuwa akiwaniwa na klabu kadhaa Ulaya.
Msimu uliopita alicheza vizuri Ajax, akifunga mabao 10 na kuseti kadhaa na hivi karibuni baba yake alisema anapenda mwanawe abaki Uholanzi kwa maendeleo yake.
"Mimi binafsi nimemuambia labda ni bora kubaki kwa mwaka mmoja zaidi Ajax, ili kupita hatua kilomita kadhaa, kuwa muhimu kwa timu," alisema Kluivertakizungumza na ESPN.
Kwenda kwake Roma ni pigo kwa kocha wa Man United, Jose Mourinho, ambaye inafahamika anampenda Kluivert na amekuwa akitaka kumsajili chipukizi huyo.
Mourinho alipigwa picha akimkumbatia mchezaji huyo baada ya fainali ya Europa League ambayo Man United waliifunga Ajax 2-0 mjini Stockholm.
0 comments:
Post a Comment