Harry Kane amesaini mkataba mpya wa miaka sita na Tottenham Hotspur PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MSHAMBULIAJI Harry Kane amesaini mkataba mpya wa miaka sita na Tottenham ambao utamfanya aongezewe mshahara hadi Pauni Milioni 90 mwa muda wote huo.
Nahodha huyo wa England amekuwa akilipwa mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki ambao sasa atakuwa analipwa mara mbili na kupokea Pauni Milioni 15 kwa mwaka, akiingia kwenye orodha ya wachezaji wa Ligi Kuu ya England wanaolipwa vizuri.
Mwenyekiti, Daniel Levy ameendelea na jitihada zake za kuhakikisha anabaki na timu imara kwa kumtia pingu na Kane akitoka kumsainisha mkataba mpya wa miaka mitano kocha Mauricio Pochettino.
0 comments:
Post a Comment