Cleveland, OHIO
TIMU ya Golden State Warriors alfajiri ya leo imetwaa ubingwa wa mpira wa kikapu Marekani (NBA) ikiwa nyumbani kwa wapinzani wao Cleveland Cavaliers baada ya kushinda kwa pointi 108-85.
Warriors wametwaa ubingwa huo katika mchezo wa nne tu na wala hawakufika katika mchezo saba kwani ushindi iliyoupata leo umewafanya kuongoza kwa michezo 4-0.
Cleveland wamepigwa ‘sweep’ kwani hawakupata ushindi katika mchezo wowote wa fainali ya mwaka huu ambayo wanakutana kwa mara ya nne mfululizo.
Stephen Curry amefunga pointi 37 huku Kevin Durant akiongeza pointi 20 na kuiweezsha Warriors kushinda mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Quicken Loans Arena uliopo Cleveland, Ohio, Marekani.
Warriors hawakujali kama wanacheza ugenini, walichokifanya ni kupambana kwa nguvu zote na kupata ushindi huo huku Cleveland wakiongozwa na LeBron James wakionekana kutaka kusawazisha.
Kevin Durant pamoja na kufunga pointi 20, zikiwemo tatu mara mbili pia ameibuka MVP. Nyota wa Cavs, LeBron James, ambaye anaweza kuwa amecheza mechi yake ya mwisho kwa Cleveland baada ya mechi alisema ameumia mkono.
Katika michezo mitatu ya nyuma, Warriors waliupata ushindi wa 110-102, 122-103 na124-114. Katika fainali tatu walizokutana huko nyuma, Warriors imeshinda mara mbili na Cleveland ikashinda mara moja.
Mabingwa; Wachezaji wa Golden State Warriors wakiwa na taji lao NBA na Medali zao za Dhahabu baada ya ushindi wa pointi 108-85, dhidi ya Cleveland Cavaliers ambao unakuwa wa nne mfululizo katika fainali za Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment