KOCHA mpya wa Arsenal, Unai Emery amepata ratiba ngumu ya mwanzo mwa msimu wa Ligi Kuu ya England akipangiwa vigogo mfululizo Manchester City na Chelsea.
Ratiba ya Ligi Kuu ya England msimu wa 2018-2019 imetoka leo na mabingwa watetezi, watasafiri kwenda Uwanja wa Emirates kumenyana na Arsenal katika mchezo wa ufunguzi. The Gunners watasafiri kwenda Uwanja wa Stamford Bridge kuwafuata Chelsea wiki moja baadaye.
Mchezo wa kwanza wa Tottenham kwenye Uwanja wao mpya wa White Hart Lane utakuwa ni dhidi ya Liverpool wikiendi ya Septemba 15.
Unai Emery amepangiwa vigogo mfululizo Manchester City na Chelsea katika mechi mbili za mwanzo za Ligi Kuu England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Mbali na mechi kati ya City na Arsenal, ufunguzi wa msimu wa Ligi Kuu ya England utashuhudia pia Manchester United ikiwakaribisha Leicester, Chelsea wakiifuata Huddersfield, Liverpool wakimenyana na West Ham na Tottenham wakisafiri kuwafuata Newcastle.
Mtanange wa Arsenal dhidi ya Man City unazima sera za muda mrefu za Ligi Kuu ya England kutokutanisha timu zilizomaliza nafasi sita za juu msimu uliotangulia katika mechi za kwanza za msimu mpya.
Baada ya kumenyana na mabingwa, Man City, Arsenal watasafiri kwenda Stamford Bridge kumenyana na Chelsea katika mechi yao ya pili wakiwa na kocha mpya, Emery.
Mechi ya kwanza ya nyumbani ya Tottenham dhidi ya Fulham Agosti 18 itachezwa Uwanja wa Wembley wakati haua za mwisho za ukarabati wa Uwanja zikikamilishwa, klabu hiyo imethibitisha leo.
Spurs baadaye watasafiri kwa mechi za ugenini dhidi ya Manchester United na Watford kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa kati ya Septemba 3 na Septemba 11.
0 comments:
Post a Comment