// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AMRI SAID ‘STAM’ AVAA VIATU VYA NDAYIRAGIJJE MBAO FC, AMUACHIA MATOLA LIPULI YAKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AMRI SAID ‘STAM’ AVAA VIATU VYA NDAYIRAGIJJE MBAO FC, AMUACHIA MATOLA LIPULI YAKE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, June 04, 2018

    AMRI SAID ‘STAM’ AVAA VIATU VYA NDAYIRAGIJJE MBAO FC, AMUACHIA MATOLA LIPULI YAKE

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Mbao FC ya Mwanza leo imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha Amri Said ‘Stam’ kuifundisha timu hiyo kwa msimu ujao.
    Mkataba huo umesainiwa leo kwenye ofisi za wadhamini wakuu wa Mbao FC, GF Trucks &Equipment Limited, Vingunguti mjini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Imran Karmali.
    Na ni Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi aliyesaini mkataba huo na Amri Said leo mjini Dar es Salaam.
    Amri Said, beki wa zamani wa Maji Maji ya Songea na Simba SC ya Dar es Salaam anachukua nafasi ya kocha wa muda wa, Fulgence Novatus aliyekuwa anaiongoza timu hiyo baada ya kuondokewa na aliyekuwa kocha wake Mkuu, Mrundi Etienne Ndayiragijje.
    Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi (kushoto) akipeana mkono na Amri Said baada ya kusaini mkataba leo

    Amri Said (wa kulia) akiwa na viongozi na wafadhili wa Mbao FC leo Vingunguti, Dar es Salaam

    Ndayiragijje ambaye aliiongoza kwa mafanikio Mbao FC kwa msimu mmoja na nusu ikiwemo kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) amejiunga na Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC). 
    Amri anajiunga na Mbao FC akitokea Lipuli ya Iringa ambako alikuwa kocha Msaidizi mbele ya Suleiman Matola mchezaji mwenzake na Nahodha wake wa zamani SImba SC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AMRI SAID ‘STAM’ AVAA VIATU VYA NDAYIRAGIJJE MBAO FC, AMUACHIA MATOLA LIPULI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top