KOCHA Gareth Southgate ametaja kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 cha timu ya taifa ya England kilichosheheni wazoefu kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.
Ndani ya kikosi hicho, kocha huyo amemjumuisha beki mkongwe mwenye umri wa miaka 32, Gary Cahill wa Chelsea ambaye ameichezea mechi 58 timu hiyo.
Southgate pia amewaita wote, Trent Alexander-Arnold na Kieran Trippier kwa ajlii ya beki ya kulia.
Alexander-Arnold mwenye umri wa miaka 19, amechukuliwa kwenye kikosi hicho baada ya kazi nzuri akiwa na Liverpool kwenye michuano yote, Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kati ya wachezaji aliowaita Southgate watano, Jordan Henderson, Raheem Sterling, Danny Welbeck, Phil Jones na Cahill walikuwepo kwenye fainali zilizopita za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Hakuna kati yao amewahi kushinda mechi ya Kombe la Dunia.
KIKOSI KAMILI CHA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND;
0 comments:
Post a Comment