Na Mwandishi Wetu, GENK
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta usiku huu ameisaidia timu yake, KRC Genk kupata tiketi ya kucheza michuano ya Europa League baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zulte Waregem Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
Nahodha huyo wa Taifa Stars leo amefunga bao la kwanza dakika ya 18, akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, kinda wa umri wa miaka 23, Leandro Trossard, kabla ya beki Mfinland, Jere Uronen kufunga la pili dakika ya 28 akimalizia pasi ya kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero.
Kwa ushindi huo, Genk wamejihakikishia tena kucheza michuano ya Europa League mwakani, huku Samatta akielekea kucheza michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo tangu ajiunge na timu hiyo.
Mbwana Samatta akishangilia baada ya kuifungia bao la kwanza KRC Genk ikipata tiketi ya kucheza Europa League
Samatta leo amefikisha mabao 26 akicheza mechi yake ya 90 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kikosi cha KRC Genk leo kilikuwa: Vukovic, Uronen, Colley, Aidoo, Mata, Seck, Malinovskyi/Berge dk75, Pozuelo/Writers dk84, Trossard, Ndongala/Buffalo dk60 na Samatta.
Zulte-Waregem : Bossut, Fauw, Baudry, Harbaoui, Kaya/Marcq dk45, De Pauw/Saponjic dk45, Walsh, De Sart, Bjordal, Bongonda/Coopman dk74 na Olayinka.

0 comments:
Post a Comment