Mohamed Salah amevunja rekodi ya mabao katika Ligi Kuu ya England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MABAO 32 aliyofunga Mohamed Salah katika mchezo wa mwisho wa Liverpool jana ikiibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Brighton and Hove Albion yanamaanisha amevunja rekodi katika Ligi Kuu ya England.
Bao la rekodi la Salah lilipatikana dakika ya 26, wakati alipopiga shuti lake la kwanza kwenye eneo la penalti baada ya pasi ya Dominic Solanke.
Mmisri huyo amevunja rekodi ya muda mrefu ya mabao 31, iliyokuwa inashikiliwa kwa pamoja na Alan Shearer (1995-1996), Cristiano Ronaldo (2007-2008) na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Luis Suarez (2013-2014).
Shearer anaendelea kushikilia rekodi ya mabao mengi katika mechi 42 kwa msimu kwa pamoja na Andy Cole. Wachezaji hao wa zamani wa kimataifa wa England walifunga mabao 34 msimu wa 1993-1994 kwa Shearer na 1994-1995 kwa Cole.
Wakati huo huo: Mohamed Salah jana alikamilisha tuzo tatu kwa mpigo baada ya kuthibitishwa ndiye Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England wa Msimu.
Salah ambaye tayari ameshinda tuzo za Chama cha Waandishi wa Habari wa Soka na Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA, amewapiku Kevin De Bruyne, David de Gea, Harry Kane, Raheem Sterling na James Tarkowski kuwa Mchezaji Bora wa Msimu England.
0 comments:
Post a Comment