// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC WAACHANA NA MSHAMBULIAJI WAO MGHANA BERNARD ARTHUR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC WAACHANA NA MSHAMBULIAJI WAO MGHANA BERNARD ARTHUR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, May 15, 2018

    AZAM FC WAACHANA NA MSHAMBULIAJI WAO MGHANA BERNARD ARTHUR

    Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI Mghana, Bernard Arthur amevunja mkataba na klabu ya Azam FC ya Dar es Saalam baada ya nusu msimu tu wa kuwa na timu hiyo ya bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake.   
    Arthur ambaye kwa Ghana mara ya mwisho alichezea Liberty Professionals ya kwo, amevunja mkataba na timu hiyo ya Dar es Salaam kutokana na kupewa muda wa kutosha wa kucheza.
    Licha ya kuwa na mwanzo mzuri kwenye Ligi Kuu ya Vodacpm Tanzania Bara akianza na kufunga bao katika mechi yake ya kwanza, Mghana huyo akatofautiana na kocha mpya Mromania, Cioaba Aristica aliyeanza kumuweka benchi mchezaji huyo.
    Bernard Arthur amevunja mkataba na klabu ya Azam FC ya Dar es Saalam baada ya nusu msimu tu  

    Na baada ya kuondolewa kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa klabu, Abdul Mohammed ambaye ndiye alimsajil Mghana huyo na baadaye kutimuliwa kwa kocha Mromania Aristica Cioaba, Arthur akapoteza kabisa matumaini ya kubaki Chamazi.
    Arthur mwenye umri wa miaka 21, amefunga mabao sita katika mechi zake tano za mwanzoni na Azam FC kabla ya kuja ‘kuzimika’ siku chache baada ya kuanza kusugua benchi.
    Bernard alikuwa mfungaji tegemeo na wa mabao mengi wa Liberty Professionals mwishoni mwa msimu uliopita kabla ya kujiunga na Azam FC Januari mwaka huu kwa mkataba wa miaka miwili, akichukua nafasi ya Mghana mwenzake, Yahya Mohammed aliyevunjiwa mkataba pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC WAACHANA NA MSHAMBULIAJI WAO MGHANA BERNARD ARTHUR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top