Na Mwandishi Wetu, MAZGHAN
WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku wa jana amecheza kwa dakika zote 90, timu yake, Difaa Hassan El- Jadida ikichapwa mabao 2-0 na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi, El Jadida mjini Mazghan.
Mshambuliaji Mkongo mwenye umri wa miaka 24, Ben Malango Ngita aliifungia bao la kwanza TP Mazembe dakika ya 51 akimalizia pasi ya Adama Traore kabla ya naye kumsetia Abdoulaye Sissoko kuifungia timu ya Lubumbashi bao la pili dakika ya 55.
Simon Msuva wa tatu kushoto na wachezaji wenzake wa Difaa Hassan El Jadida kabla ya mechi jana
Kikosi cha TP Mazembe kabla ya mchezo wa jana Uakishinda 2-0 ugenini
Hiyo inakuwa mechi ya pili mfululizo Difaa Hassan El- Jadida kucheza bila kushinda katika kundi lake, baada ya kulazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, MC Alger katika mechi ya ufunguzi Mei 4 mjini Algiers.
Mechi nyingine za jana; KCCA iliichapa 2-0 Al Ahly ya Misri Uwanja wa Nelson Mandela mjini Kampala, Uganda, Mbabane Swallows iliichapa 1-0 Primiero de Agosto, Esperance ikaikung’uta 4-1 Township Rollers, MC Alger wakaichapa 1-0 ES Setif katika mechi ya mahasimu wa Alger na mabingwa watetezi, Wydad Casablanca wakaicharaza 3-0 Togo Port.
Michuano hiyo itaendelea kwa mchezo mmoja tu leo, Etoile du Sahel wakiikaribisha Zesco United ya kocha George Lwandamina kuanzia Saa 4: 00 usiku nchini Tunisia.

0 comments:
Post a Comment