Kundi B; RS Berkane (Morocco), El Masry (Misri), UD Songo (Msumbiji) na El Hilal (Sudan).
Kundi C; Enyimba (Nigeria), Williamsville (Ivory Coast), CARA (Kongo) na Djoliba (Mali)
Kundi D; Rayon Sports (Rwanda), USM Alger (Algeria), Yanga SC (Tanzania) na Gor Mahia (Kenya).
Na Mwandishi Wetu, CAIRO
YANGA SC imepangwa Kundi D pamoja na USM Alger ya Algeria, Rayon Sport ya Rwanda na Gor Mahia ya Kenya katika hatua ya 16 Bora ya Kombe Shirikisho Afrika.
Katika Droo ya hatua ya makundi iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri Kundi A lina timu za ASEC Mimosa ya Ivory Coast, Raja Club Athletic, maarufu Raja Casablanca ya Morocco, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Aduana Stars ya Ghana.
Kundi B linaundwa na RS Berkane ya Morocco, Al Masry ya Misri, UD Songo ya Msumbiji na El Hilal ya Sudan, wakati Kundi C lina timu za CARA ya Kongo, Enyimba ya Nigeria, Williamsville na Djoliba ya Mali.
Droo hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa CAF, Amr Fahmy na Katibu Msaidizi, Anthony Baffoe.
Yanga itaanzia ugenini hatua ya makundi kwa kumenyana na USMA Alger nchini Algeria Mei 6, kabla ya kumenyana na Rayon Sport mjini Dar es Salaam Mei 16 na itakamilisha mechi za mzunguko wa kwanza kwa kuwafuata Gor Mahia mjini Nairobi Julai 18.
Mzunguko wa pili Yanga itaanzia nyumbani Julai 29 na Gor Mahia, kabla ya kuwakaribisha na USMA Alger Agosti 19 na kwenda kumalizia ugenini Agosti 29 na Rayon.
RATIBA YA MECHI ZA YANGA KUNDI D
Mei 6, 2018: USMA v Yanga, Algiers
Mei 16, 2018: Yanga v Rayon, Dar Es Salaam
Julai 18, 2018: Gor Mahia v Yanga, Nairobi
----------------------------------------
Julai 29, 2018: Yanga v Gor Mahia, Dar es Salaam
Agosti 19, 2018: Yanga v USMA, Dar es Salaam
Agosti 29, 2018: Rayon v Yanga, Kigali
0 comments:
Post a Comment