• HABARI MPYA

        Tuesday, April 24, 2018

        MAGETI KUFUNGULIWA MAPEMA MECHI YA SIMBA NA YANGA JUMAPILI

        Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
        MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga Jumapili Aprili 29,2018 uliopangwa kuchezwa saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa Tiketi zinaendelea kuuzwa kupitia Selcom.
        Yeyote anayetaka kununua tiketi hizo kupitia Selcom anachotakiwa kufanya ni kujaza pesa kwenye kadi yake ya Selcom ambayo inamuwezesha kuweza kununua tiketi hizo kupitia simu ya mkononi.
        Mageti yanatarajia kufunguliwa mapema kuanzia saa 2 asubuhi ambapo vyakula na vinywaji vitapatikana ndani.
        Jeshi la Polisi limehakikisha ulinzi utakua wa hali ya juu na kuwatahadharisha wale wote wenye nia ya kufanya vitendo vya uovu.
        Mamlaka ya Uwanja imethibitisha kuongezeka kwa camera za Uwanjani ambapo sasa zimefikia 109 ambazo zitakuwa zinafuatilia matukio yote.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: MAGETI KUFUNGULIWA MAPEMA MECHI YA SIMBA NA YANGA JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry