TIMU ya Liverpool itakutana na Roma ya Italia katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kuelekea kutwaa taji la kwanza la michuano hiyo baada ya miaka 11.
Liverpool itakutana na Roma ya Italia katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kikosi cha Jurgen Klopp kitawakaribisha wababe wa Serie A Uwanja wa Anfield katika Nusu Fainali ya kwanza Aprili 24 au 25, kabla ya kusafiri kwa mchezo wa marudiano Uwanja wa Olimpico Mei 1 au 2.
Real Madrid itaanzia nyumbani dhidi ya Bayern Munich katika Nusu Fainali nyingine kali ya michuano hiyo kabla ya kusafiri kwa mchezo wa marudiano Ujerumani.
Liverpool imefika Nusu Fainali baada ya kuwatoa vinara wa Ligi Kuu ya England Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1, ikishinda 3-0 Anfield na 2-1 Etihad.
Fainali ya michuano hiyo itafanyika Uwanja wa NSC Olimpiyskiy mjini Kiev, Ukraine Jumamosi ya Mei 26.
Liverpool itakutana na Roma ya Italia katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment