• HABARI MPYA

        Friday, April 20, 2018

        KOCHA AJERUHIWA MECHI YA MAHASIMU UTURUKI YAVUNJIKA

        NUSU Fainali ya Kombe la Uturuki baina ya Fenerbahce na Besiktas ilivunjika jana baada ya vurugu zilizodababisha kocha wa wageni, Senol Gunes kujeruhiwa kichwani.
        Mechi ilimalizika baada ya Senol Gunes kupigwa na kitu kizito kichwani kutoka jukwaani.
        Mechi hiyo ya mahasimu wa jiji la Istanbul iliyopigwa Fenerbahce, ilisimama mara kadhaa jana kutokana na vurugu, kabla ya kusitishwa kabisa dakika ya 58 timu hizo zikiwa hazijafungana.
        Gunes alianguka chini baada ya kupigwa na kitu hicho kizito kichwani kabla ya kukimbizwa hospitali, ambako alishonwa nyuzi tano, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya Habari.

        Senol Gunes akigalagala chini baada ya kujeruhiwa na kitu kizito PICHA ZAIDI GONGA HAPA


        Kocha Msaidizi, Erdinc Gultekin pia alimwagikiwa damu usoni baada ya vurugu zilizohusisha wachezaji na viongozi wa timu zote mbilif.
        Beki wa Besiktas, Pepe alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya nusu saa. Mechi ya kwanza timu hizo zilifungana 2-2.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: KOCHA AJERUHIWA MECHI YA MAHASIMU UTURUKI YAVUNJIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry