Arsenal ya England itamenyana na Atletico Madrid ya Hispania katika Nusu Fainali ya michuano ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Arsenal imepangwa kama timu ya nyumbani katika droo ya Nusu Fainali iliyofanyika leo, maana yake wataanzia nyumbani Uwanja wa Emirates.
Mechi ya kwanza itachezwa Aprili 26 Emirates, wakati marudiano yatafuatia Uwanja wa Wanda Metropolitano Mei 3.
Mechi hizo mbili dhidi ya Atletico Madrid zitafanyika katikati ya mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United.
Na hiyo itakuwa mechi ya kwanza ya ushindani kuwakutanisha Wenger na bosi wa Atletico, Diego Simeone kwa mara ya kwanza kama makocha.
0 comments:
Post a Comment