// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA YAPEWA WAHABESHI WALIOING’OA ZAMALEK KOMBE LA SHIRIKISHO, MECHI YA KWANZA DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA YAPEWA WAHABESHI WALIOING’OA ZAMALEK KOMBE LA SHIRIKISHO, MECHI YA KWANZA DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 21, 2018

    YANGA YAPEWA WAHABESHI WALIOING’OA ZAMALEK KOMBE LA SHIRIKISHO, MECHI YA KWANZA DAR

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    YANGA SC itamenyana na Welayta Dicha ya Ethiopia katika mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Welayta Dicha watakuwa wanakwenda Tanzania kwa mara ya pili mwaka huu, baada ya Februari kuja kucheza na na Zimamoto ya Zanzibar na kushinda kwa jumla ya mabao 2-1, ikitoa sare ya 1-1 Uwanja wa Amaan, kabla ya kushinda 1-0 Erthiopia.
    Hiyo ni baada ya droo iliyopangwa leo mjini Cairo, Misri na Yanga SC wataanzia nyumbani kati ya Aprili 6 na 8 kabla ya mechi ya marudiano mjini Addis Ababa kati ya Aprili 17 na 18, mwaka huu.


    Yanga SC imeangukia kwenye mchujo huo baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 2-1 iliyofungwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya sare 0-0 kwenye mchezo wa marudiano na wenyeji, Township Rollers Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana.
    Welayta Dicha imefika hatua hii baada ya kuitoa Zamalek ya Misri kwa penalti 4-3 baada ya sare ya jumla ya 3-3, kila timu ikishinda 2-1 nyumbani kwake.
    Katika Raundi ya Awali ambayo Yanga SC iliitoa Saint Louis Suns United ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Dar es Salaam na sare ya 1-1 Mahe, Welayta Dicha iliitoa Zimamoto ya Zanzibar kwa jumla ya mabao 2-1, ikitoa sare ya 1-1 Uwanja wa Amaan, kabla ya kushinda 1-0 Erthiopia.
    Huu ni mwaka wa tatu mfululizo, Yanga inaangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na mara ya nne kwa ujumla kihiostoria.
    Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2007 ilipotolewa na na El Merreikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 2-0 iliyofungwa Khartoum baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
    Iliingia kwenye kapu hilo baada ya kutolewa na  Esperance ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mabao 3-0 iliyofungwa mjini Tunis, baada ya sare 0-0 Mwanza.
    Mwaka pekee Yanga ilifuzu hatua ya makundi Kombe la Shrikisho Afrika baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa ni 2016, ilipoitoa Sagrada Esperança ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 1-0 Angola.
    Hiyo ilikuwa baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kwenda kufungwa 2-1 Alexandria.
    Katika hatua ya makundi, Yanga ilipangwa Kundi moja na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), MO Bejaia ya Algeria na Medeama SC ya Ghana. 
    Yanga ilishinda mechi moja tu dhidi ya MO Bejaia 1-0 na sare ya 1-1 na Medeama Dar es Salaam huku mechi nyingine zote nne ikifungwa, zikiwemo mbili za nyumbani na ugenini na TP Mazembe.
    Mwaka jana pia Yanga baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia kwa mabao ya ugenini, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na 0-0 Lusaka, ikaenda kutolewa na MC Alger ya Algeria kwa jumla ya mabao 4-1 kwenye mchujo wa kuwania tiketi ya hatua ya makundi Kombe la Shirikisho, ikishinda 1-0 Dar es Sakaam na kufungwa 4-0 Algiers.


    Welayta Dicha imeitoa Zamalek ya Misri kwa penalti 4-3 baada ya sare ya jumla ya 3-3, kila timu ikishinda 2-1 nyumbani kwake


    RATIBA KAMILI KOMBE LA SHIRIKISHO
    Zanaco (Zambia) v Raja Casablanca (Morocco)
    AS Vita (DRC) v CS La Mancha (Kongo Brazaville)
    St George (Ethiopia) v CARA Brazzaville (DRC)
    El Hilal (Sudan) v Akwa United (Nigeria)
    SuperSport United (Afrika Kusini) v Gor Mahia (Kenya)
    Al-Hilal Al-Ubayyid (Sudan) v UD Songo (Msumbiji)
    USM Alger (Algeria) v Plateau United (Nigeria)
    Enyimba (Nigeria) v Bidvest Wits (Afrika Kusini)
    Aduana Stars (Ghana) v Fosa Juniors (Madagascar)
    Young Africans (Tanzania) v Welayta Dicha (Ethiopia)
    Generation Foot (Senegal) v RS Berkane (Morocco)
    CF Mounana (Gabon) v Al-Masry (Misri)
    ASEC Mimosas (Ivory Coast) v CR Belouizdad (Algeria)
    Williamsville AC (Ivory Coast) v Deportivo Niefang (Equatorial Guinea)
    MFM (Nigeria) v Djoliba (Mali)
    Rayon Sports (Rwanda) v Costa do Sol (Msumbiji)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA YAPEWA WAHABESHI WALIOING’OA ZAMALEK KOMBE LA SHIRIKISHO, MECHI YA KWANZA DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top