// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TWIGA STARS YAINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA AFCON, TAIFA STARS KUWAFUTAA ALGERIA WIKI IJAYO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TWIGA STARS YAINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA AFCON, TAIFA STARS KUWAFUTAA ALGERIA WIKI IJAYO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 13, 2018

    TWIGA STARS YAINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA AFCON, TAIFA STARS KUWAFUTAA ALGERIA WIKI IJAYO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars imeingia kambini katika Hostel za Makao Makuu ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT Mlalakuwa) kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake AFCON 2018 nchini Ghana.
    Twiga Stars itacheza dhidi ya Zambia (She Polopolo) Aprili 4, 2018 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na marudiano kufanyika April 8, 2018 jijini Lusaka nchini Zambia.
    Mshindi wa jumla kwa raundi hii atacheza na mshindi kati ya Namibia v Zimbabwe mwezi Mei, na atakayeibuka mshindi atafuzu moja kwa moja kwa Fainali hizo za Wanawake Afrika.
    Taifa Stars inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kalenda ya FIFA inayoanza Machi 19 – 27, 2018 dhidi ya timu za Taifa za Algeria na DR Congo.
    Stars itasafiri kuelekea jijini Algiers kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Algeria Machi 22, 2018 na baada ya mchezo huo dhidi ya Algeria, Taifa Stars itarejea nyumbani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Congo DR Machi 27, 208 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS YAINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA AFCON, TAIFA STARS KUWAFUTAA ALGERIA WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top