// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STAND UNITED YATANGULIA NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STAND UNITED YATANGULIA NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 30, 2018

    STAND UNITED YATANGULIA NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION

    Na Alexander Shijja, SHINYANGA
    TIMU ya Stand United imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Njombe Mji FC jioni ya leo Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
    Shukrani kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Abdul Swamad dakika ya 12 akimalizia krosi ya Vitalis Mayanga ambaye naye alipokea pasi ya beki Eric Mulilo aliyepanda vizuri upande wa kulia kusaidia mashambulizi.
    Stand United ilimaliza pungufu mchezo huol, baada ya Nahodha wake, Erick Mulilo kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 80 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
    Stand sasa itakutana na mshindi kati ya Azam FC na Mtibwa Sugar katika Nusu Fainali kati ya Aprili 16 na 18 wakisariri kwenda kucheza ugenini.
    Robo Fainali za Azam Sports Federation Cup zitaendelea kesho, Tanzania Prisons wakiwakaribisha JKT Tanzania Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya kuanzia Saa 10:00 jioni kabla ya Azam FC kuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mechi za Robo Fainali ya Azam Sports Federation zitakamilishwa Jumapili kwa Singida United kuwakaribisha Yanga SC Uwanja wa Namfua mjini Singida.
    Kikosi cha Singida United kilikuwa; Mohammed Makaka, Erick Mulilo, Aaron Michael, Miraj Maka, Ally Ally, Bigirimana Mlaise, Abdul Swamad, Vitalis Mayanga, Abdallah Juma, Ndikumana Suleiman na Adam Ismail.
    Njombe Mji FC; Rajab Mbululo, Joshua Thawe, John Sigala, Mark Mwambungulu, Laban kamboole, Aden Chepa, Francis Anyengisye, Behewa Ally, Notikel Masasi, Claude Migenge na Willy Mgaya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STAND UNITED YATANGULIA NUSU FAINALI AZAM SPORTS FEDERATION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top