Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa kwanza Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC ya Tanzania na Al Masry ya Misri uliochezwa Jumatano wiki hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeingiza jumla ya Sh. 85,045,000.
Kiasi hicho cha fedha kimetokana na jumla ya watazamaji 14,798 waliojitokeza kuushuhudia mchezo huo uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.
Katika watazamaji hao 14,798 ni 250 tu walioketi jukwaa la VIP A ambako kiingilio chake kilikuwa Sh. 20,000 na kupatikana jumla ya shilingi 5,000,000, watazamaji 557 waliketi VIP B na C ambako viingilio vyake vilikuwa Sh 15,000 na kapatikana jumla ya Sh 8,355,000.
Sehemu ya mashabiki wa Simba waliojitokeza Uwanja wa Taifa juzi timu yao ikimenyana na Al Masry
Kwenye majukwa ya rangi ya Machungwa, Bluu na Kijani ndiko waliingia watazamaji wengi zaidi, 13,644 kwa kiingilio cha Sh. 5,000 ambako zimepatikana jumla ya Sh. 68,220,000.
Katika fedha hizo Sh. 12,972,966.10 imekatwa Kodi (VAT), 5,017,655.00 imeenda kwa Selcom waliokuwa wakikusanya mapato, TFF wamepata Sh. 3,352,718.94, Uwanja Sh. 10,058,156.83, Gharama za mchezo Sh. 6,034,894.10, BMT 670,543.79 na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limepata Sh. 3,352,718.94 wakati klabu ya Simba, imepata Sh. 43,585,346.28.

0 comments:
Post a Comment