Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta (katikati) akifurahi na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Taifa Stars bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji kiwa na Simon Msuva wa Difaa Hassan El Jadidi ya Morocco
Mbwana Samatta akikimbia baada ya kutikisa nyavu za The Leopard (Chui) wa Kongo
Wanaomfuata nyuma ni Ibrahim Ajib (kulia) wa Yanga ya Dar es Salaam na Simon Msuva
Mfungaji wa bao la pili la Taifa Stars, Shiza Kichuya akishangilia baada ya kufunga
Kiungo wa Simba ya Tanzania, Shiza Kichuya akitembea kwa madaha baada ya kufunga
Mgongoni kwa Mbwana Samatta ni Shiza Kichuya baada ya kufunga bao la pili
Mashabiki wakishangilia ushindi wa Taifa Stars leo
Mashabiki wa Tanzania walikuwa wenye furaha leo baada ya mabao hayo ya kipindi cha pili
Tuesday, March 27, 2018
- Blogger Comments
- Facebook Comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment