Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
REFA Florentina Zablon wa Dodoma ndiye atachezesha mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji, Simba na Stand United ya Shinyanga kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Zablon aliyechezesha mechi nyingine ya Ligi Kuu jana Uwanja wa Nangwanda, Sijaona mjini Mtwara wenyeji, Ndanda wakifungwa 2-1 na Yanga, kesho atasaidiwa na Ferdinand Chacha na Mashaka Mandemwa wote wa Mwanza.
Refa wa akiba kesho atakuwa Gelmina Simon wa Dar es Salaam na kamishna wa mechi anatoka Arusha,Peter Temu.
Wakati huo huo: Droo ya Robo Fainali ya Azam Sports Federation inatarajiwa kufanyika kesho Saa 5:00 asubuhi Makao Makuu ya Azam TV, wadhamini wa mashindano hayo, Tabata TIOT, Dar es Salaam.
Timu zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo ni Yanga SC, Azam FC za Dar es Salaam, Singida United ya Singida, Njombe Mji ya Njombe, Mtibwa Sugar ya Morogoro, Tanzania Prisons ya Mbeya, Stand United ya Shinyanga na JKT Tanzania ya Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment