MSHAMBULIAJI Neymar amewasili nchini Brazil jana akiwa kwenye kiti cha walemavu kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake — huku nyota huyo wa Paris Saint-Germain akiwa hatarini kutocheza fainali za Kombe la Dunia katikati ya mwaka nchini Urusi.
Mbrazil huyo alihitaji msaada wa wasaidizi wa Uwanja wa Ndege wakat anawasili mjini Rio de Janeiro na kifundo chake cha mguu wa kulia kilionekana kimefungwa wakati anasukumwa eneo la Uwanja wa Ndege.
Neymar mara moja atasafiri kwenda Belo Horizonte, ambako ndiko atafanyiwa upasuaji wa maumivu yake aliyoyapata Jumamosi iliyopita.
Amevunjika mfupa wa kifundo chake cha mguu katika mechi ya Jumapili timu yake, PSG ikishinda 3-0 dhidi ya Marseille.
Awali PSG walidhani hayatakuwa maumivu makubwa, lakini nyota wao sasa anaelekea kukosa sehemu yote ya msimu iliyobaki hadi Fainali za Kombe la Dunia, Urusi.
Awali PSG walidhani hayatakuwa maumivu makubwa, lakini nyota wao sasa anaelekea kukosa sehemu yote ya msimu iliyobaki hadi Fainali za Kombe la Dunia, Urusi.
Kwa mujibu wa Daktari wa timu ya taifa ya Brazil, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kuwa nje ya Uwanja kwa hadi miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Rodrigo Lasmar, amenukuliwa na tovuti ya gazeti la O Globo la Brazil akiseam kwamba mchezaji huyo ghali zaidi duniani atakuwa nje kwa muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment