Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MAJINA ya vigogo wa soka Afrika, wakiwemo mabingwa wa Afrika 1998, Raja Casablanca yametawala katika orodha ya wapinzani wapya wa Yanga kwenye michuano ya Afrika.
Yanga SC imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.
Hiyo ni baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana.
Matokeo hayo yanamaanisha Rollers inakwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza historia hiyo kwa ushindi wa jumla wa 2-1 uliotokana na matokeo ya mchezo wa kwanza Dar es Salaam Machi 6.
Na Yanga SC itamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, ambazo ni CR Belouizdad, USM Alger za Algeria, Al-Masry ya Misri, Djoliba ya Mali, Raja Casablanca, Enyimba ya Nigeria, SuperSport United ya Afrika Kusini na Al-Hilal Al-Ubayyid ya Sudan.
Pamoja na Yanga, wapinzani wengine wa timu hizo ni AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ASEC Mimosas, Williamsville AC za Ivory Coast, Saint George ya Ethiopia, CF Mounana ya Gabon, Aduana Stars ya Ghana, Gor Mahia ya Kenya na UD Songo ya Msumbiji.
Wengine ni MFM, Plateau United za Nigeria, Rayon Sports ya Rwanda, Generation Foot ya Senegal, Bidvest Wits ya Afrika Kusini, Al-Hilal ya Sudan na Zanaco ya Zambia.
Droo ya ratiba ya mechi za mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kupangwa kesho makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

0 comments:
Post a Comment