TIMU za Borussia Dortmund na Lyon zimetolewa kwenye michuano ya Europa League usiku wa Alhamisi huku ratiba ya Robo Fainali ikitarajiwa kupangwa leo mchana.
Marseille, Lazio, Salzburg, CSKA Moscow, Sporting Lisbon na Leipzig zinaungana na wapewa nafasi kubwa kubeba taji Atletico Madrid na Arsenal kukamilisha Nane Bora za Europa League 2018.
Dortmund, mmoja wa mabingwa wa zamani wa Ulaya jana ililazimishwa sare ya 0-0 na Salzburg na kufanya watolewe kwa jumla ya mabao 2-1 waliyofungwa nyumbani.
Wachezaji wa Borussia Dortmund wakiwa wanyonge jana baada ya kutolewa Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Atletico Madrid itakuwa timu pekee kjuiwakilisha Hispania katika Nane Bora baada ya Athletic Bilbao kufungwa 2-1 nhyumbani na Marseille, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 5-2.
Lazio walionekana kuingia kwenye mtihani mgumu baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Dynamo Kiev kwenye mchezo wa kwanza, lakini mabao ya kiungo wa zamani wa Liverpool, Lucas na Stefan de Vrij yaliwapa ushindi wa 2-0.
Salzburg wakaendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika mechi ya 19 na kuwa timu ya kwanza ya Austria kufika Robo Fainali ya Europa League.
Droo ya leo inaweza kuwakutanisha na RB Leipzig, klabu ya Bundesliga yenye mdhamini mmoja na wao.
Leipzig imeingia Robo Fainali baada ya sare ya 1-1 na mabingwa wa mwaka 2008 Kombe la UEFA, Zenit St Petersburg na kufanya ushindi wa jumla wa 3-2.
0 comments:
Post a Comment